Translate

Monday, 10 August 2015

ANAGALIA WASANII10 WENYE UTAJIRI ZAIDI AFRIKA

Ni swali ambalo mara kibao limezua mjadala,  kuhusu nani bingwa wa mihela katika tasnia ya muziki afrika.  Wengi wetu tukishangaa kama wa bongo  tupo kwenye orodha hii.  Ila cha kushanga, a ni kuwa wengi wa wasanii wanaotesa sana hawapo kabisa.  Hii ikiwa imechangiwa na kutokuwepo kwa myda mrefu,  au pengine malipo ya show. Hivi ni haki kwa wengi wa wasanii wetu kuwa na jeuri ya hela wakati hawapo popote katika orodha hii?  Anagalia mwenyewe kisha  nipe maoni yako


10. Jose Chameleone, (Uganda)Tsh Billioni 50 

Anafahamika kama Joseph Mayanja.  Alizaliwa mwaka 1979na kuanza muziki miaka ya awali ya tisini.  Kipindi hicho alikuwa ni mc qa disco vumbi kule kwao,  kwenye klabu moja hivi inaitwa maganjo night club. Alihama na kuelekea kenya aliposaini mkataba na Studio ya ogopa djs na kuachia vibao kama dorotia na jamila.  Jose Chameleone anamiliki gari la Cadillac escalade ambalo ni sawia na the beast gari analotumia  rais wa marekani., hii ni pamoja na mali nyingine ikiwemo helicopter moja. Inakariwa kuwa show moja Chameleone ni takribani millioni ishirini. 

9. Banky W, (Nigeria)Naira 1.8 billion


Banky W ni msanii wa nigeria ambaye jina lake halisi ni Wellington Olubankole. Alizaliwa kule lagos mwaka 1981 kuanza kukyza kipaji chake kanisani... Baadaye banky w aliondoka nigeria kupata shahada la uhandisi, na baadaye kurejea nyumbani na kujikita katika tasnia ya muziki wa rnb. Yeye ndiye mwakilishi wa kampuni ya mawasiliano ya etisalat,  na pia uso wake unatumika katika matangazo ya simu ya samsung katika africa magharibi. Pamoja na muziki endorsements mbali mbali pia zimamwingizia kiwango kikubwa tu cha hela. Wengi wakimfahamu kama king of African rnb. Banky W pia ameanzisha mradi ninafsi wa kuwapa elimu watoto werevu kutoka jamii maskini

8. Hugh Masekela ( South Africa) $ 275 million 

ni mmoja wa wasanii wakongwe zaidi barani, na haswa katika muziki wa jazz. Alizaliwa mwaka 1939 nakupewa jina hugh ramopolo masekela.  Ana tuzo nyingi na za hadhi,  ikiwemo Grammy, BBC  na zingine nyingi ikiwemo lifetime  achievement award aliyokabidhiwa na rais jacob zuma. 

7. 2face Idibia ( Nigeria) Naira 4. 5 billion 

  • 2face idibia ni mzaliwa wa nigeria ambaye jina lake halisi ni Ujah idibia innocent.  Tofauto na muziki yeyw pia ni mtunzi mwandishi,  na pia mwigizaji.  Ana album nne za muziki na pia tuzo aro aini kufikia sasa. Amewekeza sana katika sekta real estate. Na pato lake kwa kila show ni dola elfu hamsini. Pia anamiliki moja ya klabu kubwa zaidi jijini lagos.  Pamoja na haya ana ngo inayofahamika kama 2face reach out foundation kwa ajili ya kufadhili miradi mbali mbali ya maendeo.

6. Fally Ipupa ( DR Congo) 

Fally Ipupa ni mzaliwa jamhuri ya demokrasia ya kongo. Safari yake ya uimbaji ilianzia mwaka 1999 pale alipojiunga na bendi ya mkongwe wa sebene koffi olomide kama mmoja wa waimbaji wa pembeni au back up vocalists.  Aliiacha bendi mwaka 2006, na kuwa mwanamuziki binafsi. Na kuachia albim ya kwanza iliyompa umaarufu Droit Chemin. 
Fally ana tuzo kadhaa za hadhi zikiwemo kora awards na mtv,  na pia ni model wa mavazi nchini ufaransa.

Zidi kufuata peypper. Com kupata uhondo zaidi.  Na pia kupata top 5.

No comments:

Post a Comment